Ndoto hiyo ya kuota unapigana inaweza kumaanisha aidha upo kwenye mashindano au vita..
1. UPO KWENYE MASHINDANO.
Kwa namna ya kawaida, ikiwa kipo kitu Fulani ambacho kinathamani fulani, na wote mnakitamani au kukigombania ili mkipate, au mmoja anakizuia ili kisipatikane, ni rahisi kutokea kutokuelewa na mwisho wa siku mapigano, kwamfano wengine wanaishia kupigana kisa, fedha, wengine madini, wengine fursa, wengine wapenzi, na wengine thawabu n.k,
Na ndio maana utamwona mtu kama Yakobo katika biblia, alipiigania thawabu yake sana usiku kucha kwa kushindana mweleka na Yule malaika aliyemtembelea usiku..
Mwanzo 32:24 “Yakobo akakaa peke yake; na mtu mmoja akashindana naye mweleka hata alfajiri.
25 Naye alipoona ya kuwa hamshindi, alimgusa panapo uvungu wa paja lake; ukateguka uvungu wa paja la Yakobo alipokuwa akishindana naye.
26 Akasema, Niache, niende, maana kunapambazuka. Akasema, Sikuachi, usiponibariki.
27 Akamwuliza, Jina lako n’nani? Akasema, Yakobo.
28 Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda”.
Hivyo kama wewe umeokoka halafu ukaota, unapigana na mtu muda mrefu mpaka unachoka, ni mapambano tu, Hapo ni Mungu anakukumbusha habari ya Yakobo, kwamba unapaswa utafute thawabu zake kwa nguvu mpaka uzipate, kuliko kitu kingine chochote unachoweza kukitafuta katika hii dunia. Hiyo ndio tafsiri ya kwanza.
Tafsiri ya pili: Kuota unapigana ni ishara ya vita.
Wakati mwingine, watu wanaweza kupigana, si kwa ajili wanagombania kitu Fulani, hapana, bali ni kwa ajili ya chuki, wivu, fitna, kiburi, n.k..Lengo kuu ni kutaka kukuangamiza tu basi,
Waamuzi 8:33 “kisha itakuwa, asubuhi, mara litakapokucha jua, wewe utaamka asubuhi na mapema, na kuushambulia mji huo; tena, angalia, hapo yeye na wale watu walio pamoja naye WATAKAPOKUTOKEA NJE KUPIGANA NAWE, ndipo utapata kuwatenda kama utakavyopata nafasi”.
Lakini kama wewe hujaokoka, ni wazi kuwa upo hatarini, hivyo tahadhari hizi zichukue,
Mpe leo Yesu maisha yako ayaokoke, haijalishi wewe ni wa dini gani, au dhehebu gani, Yesu Kristo anawaokoa watu wote. Ikiwa leo utakubali kutubu dhambi zako zote kwa kumaanisha kabisa kuziacha, atakusamehe na kukukubadilisha na kukupa Roho wake, ambaye atakaa ndani yako milele..Na ndiye atakayekulinda na mipenyo yote ya ibilisi katika maisha yako, kwasababu tayari utakuwa ndani ya ulinzi wa ki-Mungu.
Rejeabiblia.com.