Nini maana ya kuota mti au miti inaanguka au inakatwa?
Kibiblia Mti unawakilisha “MTU”.
Marko 8:22 “Wakafika Bethsaida, wakamletea kipofu, wakamsihi amguse.
23 Akamshika mkono yule kipofu, akamchukua nje ya kijiji, akamtemea mate ya macho, akamwekea mikono yake, akamwuliza, Waona kitu?
24 Akatazama juu, akasema, Naona watu kama miti, inakwenda”.
Unaona hapo mstari wa 24? Miti inafananishwa na watu.
Hivyo unapoona katika ndoto Mti umeanguka nyumbani kwako, au kwenu au mahali popote,basi tafsiri yake ni kwamba kuna Mtu unayemfahamu au pengine wewe mwenyewe aidha atakwenda kufa au kushuka chini.
Na kifo hicho au kushushwa huko kunaweza kuwa kunasababishwa na shetani au Mungu mwenyewe.
Kama ni shetani, basi suluhisho ni Maombi, kwamba unapaswa uombe kwa bidii na Imani, ili roho ya mauti iondoke, na kumbuka huwezi kuivunja au kuiharibi mipango ya shetani kama wewe mwenyewe hujaokoka.
Huna budi umwamini Yesu na kuupata ufalme wa mbinguni maishani mwako ndipo uwe na mamlaka ya kubatilisha mipango yote ya Adui.
Lakini kama umeona umekatika au umeanguka na aliyeuangusha ni kama vile Mungu au Malaika wake, basi tambua kuwa ni Mungu anakwenda kukushusha chini au kukuangamiza kabisa, na hiyo mara nyingi ni kutokana na dhambi mtu anazozifanya zisizompendeza Mungu.
Tutalithibitisha hilo kwa ile ndoto Nebukadreza aliyoiota na kupewa tafsiri yake.
Tuisome,
Danieli 4:18
“Mimi, Nebukadreza, nimeiona ndoto hii; na wewe, Ee Belteshaza, eleza tafsiri yake, kwa maana wenye hekima wote wa ufalme wangu hawawezi kunijulisha tafsiri yake; bali wewe waweza, maana roho ya miungu watakatifu inakaa ndani yako.19 Ndipo Danieli, aliyeitwa jina lake Belteshaza, akashangaa kwa muda, na fikira zake zikamfadhaisha. Mfalme akajibu akasema, Ee Belteshaza, ndoto ile isikufadhaishe wala tafsiri yake. Belteshaza akajibu, akasema, Bwana wangu, ndoto hii iwapate wao wakuchukiao, na tafsiri yake iwapate adui zako.
20 Ule mti uliouona, uliokua, ukawa na nguvu, urefu wake ukafika mpaka mbinguni, na kuonekana kwake mpaka dunia yote;
21 ambao majani yake yalikuwa mazuri, na matunda yake mengi, na ndani yake chakula cha kuwatosha wote; ambao chini yake wanyama wa kondeni walikaa, na ndege wa angani walikuwa na makao yao katika matawi yake;
22 ni wewe, Ee mfalme, uliyekua, na kupata nguvu; maana ukuu wako umekua na kufika mpaka mbinguni, na mamlaka yako yamefika mpaka mwisho wa dunia.
23 Tena, kwa kuwa mfalme alimwona mlinzi, naye ni mtakatifu, akishuka kutoka mbinguni, akisema, Ukateni mti huu, mkauangamize; ila kiacheni kisiki cha shina lake katika ardhi, pamoja na pingu ya chuma na shaba, katika majani mororo ya kondeni; kikatiwe maji kwa umande wa mbinguni, na sehemu yake iwe pamoja na wanyama wa kondeni, hata nyakati saba zipite juu yake;
24 tafsiri yake ni hii, Ee mfalme, nayo ni amri yake Aliye juu, iliyomjia bwana wangu, mfalme;
25 ya kuwa utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa kondeni, nawe utalazimishwa kula majani kama ng’ombe, nawe utatiwa maji kwa umande wa mbinguni, na nyakati saba zitapita juu yako; hata utakapojua ya kuwa Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa yeye amtakaye, awaye yote.
26 Na kwa kuwa waliamuru kukiacha kisiki cha shina lake; ufalme wako utakuwa imara kwako, baada ya wewe kujua ya kuwa mbingu ndizo zinazotawala.
27 Kwa sababu hiyo, Ee mfalme, shauri langu lipate kibali kwako; ukaache dhambi zako kwa kutenda haki, ukaache maovu yako kwa kuwahurumia maskini; huenda ukapata kuzidishiwa siku zako za kukaa raha.
28 Hayo yote yakampata mfalme Nebukadreza.
29 Baada ya miezi kumi na miwili, alikuwa akitembea ndani ya jumba la kifalme katika Babeli.
30 Mfalme akanena, akasema, Mji huu sio Babeli mkubwa nilioujenga mimi, uwe kao langu la kifalme, kwa uwezo wa nguvu zangu, ili uwe utukufu wa enzi yangu?.
31 Hata neno lile lilipokuwa katika kinywa cha mfalme, sauti ilikuja kutoka mbinguni, ikisema, Ee mfalme Nebukadreza, maneno haya unaambiwa wewe; Ufalme huu umeondoka kwako.
32 Nawe utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa kondeni; utalishwa majani kama ng’ombe, na nyakati saba zitapita juu yako, hata utakapojua ya kuwa Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, awaye yote.
33 Saa iyo hiyo jambo hilo likatimizwa, likampata Nebukadreza; alifukuzwa mbali na wanadamu, akala majani kama ng’ombe, na mwili wake ulilowa maji kwa umande wa mbinguni, hata nywele zake zikakua, zikawa kama manyoya ya tai, na kucha zake kama kucha za ndege”.
Umeona hapo?, Nebukadreza yeye hakufa kwasababu kiliachwa kisiki, lakini endapo na kisiki kingeondolewa basi angekufa kabisa.
Na Mfalme Nebukadreza, alikatwa kwasababu ya dhambi zake, na si kingine, wala hakulogwa na mtu,ni Dhambi tu ndizo zilizomsababishia kukatwa.
Vile vile kama umeota Mti wako umekatika au kuanguka, basi yachunguze maisha yako na utubu. Mungu anakupenda ndio maana kakuonesha hayo. Lengo ni ili utubu.
Na kama basi sio wewe basi unajukumu la kwenda kumweleza huyo ndugu uliyeona mti wake umekatika kwamba atubu.
Ubarikiwe.
Vitabu kwa njia ya ebook > info@ndotozangu.com