Kuota upo chooni, unajisaidia haja kubwa au haja ndogo, au wakati mwingine unajiona uko peku chooni na choo ni kichafu.
Nini maana yake?
Unapoota upo chooni na unakojoa mkojo usioisha, mara nyingi inatokana na kwamba kibofu kimejaa mkojo, hivyo hiyo ni kawaida.
Lakini unapojikuta unaota upo chooni, tena wakati mwingine peku, na choo ni kichafu, hilo ni suala la kiroho na linahitaji ufumbuzi kiroho.
Kibiblia “Choo” kinawakilisha “madhabahu za miungu”.
Mahali popote panapoabudiwa miungu, iwe ni kwenye nyumba au katikati ya jamii ya watu fulani mahali hapo katika roho ni choo.
2 Wafalme 10:26 “Wakazitoa nguzo zilizokuwamo nyumbani mwa Baali, wakaziteketeza.
27 Wakaibomoa nguzo ya Baali, na kuiangusha nyumba ya Baali, wakaifanya choo hata leo”.
Kwahiyo ukiota upo chooni, angalia mahali unapoabudu aidha ni mahali panapoabudiwa miungu au sanamu, au tazama jinsi maisha yako ni wapi unapojihusisha na ibada za sanamu.
Na sanamu sio tu zile zile za kuchonga, bali hata uasherati, uzinzi, na mambo mengine yote mabaya ni ibada za sanamu.
Wakolosai 3:5 “Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu;
6 kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Mungu”.
Na kama jinsi choo kinavyotoa harufu, kadhalika “ibada za sanamu” ni harufu mbaya kwa Mungu, uasherati ni harufu mbaya kwa Mungu, uzinzi ni harufu mbaya kwa Mungu.
Neema ya Bwana iwe nasi.
Asante sana