Ndoto hii ni ndoto ambayo karibia kila mtu ulimwenguni, ataiota katika kipindi chochote cha maisha yake. Kwasababu ni ndoto kutoka kwa Mungu.
Kama wewe ni Mkristo, na katika ndoto umeona Bwana kaja na umeachwa, basi hiyo ni tahadhari kwako, Bwana anayokupa kwamba uzidi kuimarisha uhusiano wako na yeye, na ili siku ile isije ikakukuta kama mwivi.
Hivyo kama bado ni vuguvugu, hakikisha unakuwa moto!, maana kuna uwezekano wote wa parapanda ya mwisho ikalia na ukaachwa, Kama unafanya dhambi kwa siri basi ziache zote!, kama umepunguza kusoma Neno la Mungu, basi anza upya, tena kwa kasi!, kama umepunguza kukusanyika na wengine kanisani katika kufanya ibada na kusali na kufunga, basi anza kwenda kanisani kuanzia sasa. Kwasababu unyakuo upo karibu, na siku hiyo wengi wataachwa!, na uchungu mkubwa utakuwa ni kwa wale walio vuguvugu.
1Wathesalonike 5.2 “Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.
3 Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.
4 Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi.
5 Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza.
6 Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi.
7 Maana walalao usingizi hulala usiku, pia na walewao hulewa usiku.
8 Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, hali tukijivika kifuani imani na upendo, na chapeo yetu iwe tumaini la wokovu.
9 Kwa kuwa Mungu hakutuweka kwa hasira yake, bali tupate wokovu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo”.
KWA ASIYE NDANI YA IMANI.
Kama wewe haupo ndani ya wokovu (yaani hujamwamini Bwana Yesu kwa kutubu dhambi zako, na kubatizwa), unapoota ndoto ya namna hii, ni Mungu anaonyesha upendo wake kwako, hivyo hiyo ni ndoto ya tahadhari.
Anataka kukuonjesha hisia utakayoipata siku atakapokuja, halafu wewe umebaki, pale utakapoona wenzako wameenda mawinguni, na wewe umebaki hapa, katika dhiki kuu ya mpinga-Kristo. Siku hiyo itakuwa ni ya uchungu na maombolezo mengi. Hivyo hataki wewe ubaki ndio maana amekuonyesha hayo, hivyo unachotakiwa kufanya ni wewe kutubu dhambi zako na kutafuta kubatizwa, ili uwe salama siku atakapokuja.
Kwa msaada juu ya kubatizwa na kuokoka tutumie ujumbe kwenye email hii hapa chini
info@ndotozangu.com