Bwana Yesu Kristo asifiwe milele na milele…karibu tujifunze Neno la Mungu….
Ni shauku ya Mungu kila siku tuwe ni watu wa kuongeza maarifa katika kumjua yeye….
Kipindi cha injili ya Bwana Yesu akiwa duniani,kilikuwa ni kipindi chenye baraka na Neema sana,ilifika wakati sio lazima uwe mwanafunzi wake na wala alikuwa haji kukulazimisha uwe mfuasi wake ndo mana unaona mpaka anafika mwisho wa huduma yake ni watu wachache sana waliokuwa nae bega kwa bega tofauti na wale watu miatano aliowatokea baada ya kufufuka kwake…..
Wengine walikuwa hawamwelewi hivyo wanaona hawana ulazima kuendelea nae,Wengine wanapoisikia injili yake wanamuona ni mtu wa itikadi kali sana….Baadhi yao walipoambiwa hatma za maisha yao walimuona Bwana Yesu ni mtu asiyewawazia mema kabisa na kuamua kwenda zao ….
Marko 10:17-22
[17]Hata alipokuwa akitoka kwenda njiani, mtu mmoja akaja mbio, akampigia magoti, akamwuliza, Mwalimu mwema, nifanye nini nipate kuurithi uzima wa milele?[18]Yesu akamwambia, Kwa nini kuniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu.
[19]Wazijua amri, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, Usidanganye, Waheshimu baba yako na mama yako.[20]Akamwambia, Mwalimu, haya yote nimeyashika tangu utoto wangu.
[21]Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa na neno moja. Enenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.
[22]Walakini yeye akakunja uso kwa neno hilo, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi.
Ilifika kipindi hata wale viongozi wa dini wakawa hawamuelewi kabisa….wakamuona ni mtu anayetaka kuwapotosha watu, wakaanza kuidadisi injili yake wakaona inaenda tofauti na torati yao,wakaanza kutafuta mbinu za kumwangusha
Mathayo 21:23
Hata alipokwisha kuingia hekaluni, wakuu wa makuhani na wazee wa watu wakamwendea alipokuwa akifundisha, wakasema, Ni kwa amri gani unatenda mambo haya? Naye ni nani aliyekupa amri hii?
Lakini katika namna zote hizo za kutokueleweka kwake Bwana Yesu hakuacha kuwahubiria watu wake kwa kuzunguka kila mijini na vijijini ili awaokoe watu…Na hilo tumekuja kuliona likiendelea kwa uwezo mkuu baada ya kuondoka kwake,Baada ya Kanisa kupokea nguvu za Roho Mtakatifu,tunalithibitisha hilo katika Maandiko Matakatifu…..
Matendo ya Mitume 2:47
[47]wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku KWA WALE WALIOKUWA WAKIOKOLEWA.
Kanisa la kwanza Bwana aliliongeza kwa siku watu takribani elfu tatu ,walikuwa wanampokea Yesu Kristo na kubatizwa na kupokea Roho Mtakatifu….
Hata sasa Nguvu hii inatenda kazi kwa uwezo mkuu wa Bwana wetu Yesu Kristo,Wengi wanaokolewa na kupata wokovu kamili,Jiulize wewe ndugu yangu unasubiri nini hata sasa, Jiulize na wewe ni mmoja wapo katika wale wanaokolewa au waliokolewa..
Mpaka sasa huduma ya Bwana Yesu inayotenda kazi ni uokozi,,…
Luka 9:56
[56]Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa. Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine
Huu ni muda wako wa Yesu kuyaokoa maisha yako,huu ni wakati wako ya Yesu kuiokoa roho yako,kumbuka hakuna mwokozi mwingine zaidi ya Yesu Kristo,utaendelea na dhambi mpaka lini,utafanya maovu mpaka kipindi gani,wewe wakati unaendelea na mabaya yako wengine wanaokolewa na kuingia katika uzima wa Milele….
Badilika ndugu,mkabidhi Yesu njia zako leo ili akuokoe na mabaya ya ulimwengu huu yaliyopo na yatakayoikumba dunia hii,unyakuo wa watakatifu upo karibu sana,Kristo akija kulichukua kanisa lake jiulize na wewe utakuwa mmojwapo ,kwanini uendelee kuishi katika magereza ya shetani,wengi walikuwa wanaokolewa na hata sasa Yesu Kristo anaendelea kuwakoa wengi ili awape uzima wa Milele …
Saa ya wokovu ni sasa na si badae wala kesho,Tubu kwa kumaanisha kumkimbia Kristo…..
Wasambazie na wengine habari njema