Jina la mwokozi wetu Yesu Kristo litukuzwe, nakukaribisha tena katika wasaa mzuri wa kujifunza maneno ya uzima.
Katika hiki kipindi tulichofikia sisi wanadamu hapa duniani hadi siku ya leo, ni mengi sana tuliyoyaona na kuyashuhudia mengine yalikuwa mema na mengine yalikuwa mabaya ambayo haya mabaya yalipotokea yaliacha maumivu makali sana. Ambayo yalipelekea hata watu kusema KWANINI MUNGU AMERUHUSU HAYA YATOKEE kwa sababu ya maumivu hayo
Basi tutajifunza nini kinasababisha mabaya yanatupa sisi wanadamu
Tusome
Yeremia 5:20-27
[20]Tangazeni neno hili katika nyumba ya Yakobo, litangazeni katika Yuda, kusema,
[21]Sikilizeni neno hili, enyi watu wajinga msio na ufahamu; mlio na macho ila hamwoni; mlio na masikio ila hamsikii.
[22]Je! Hamniogopi mimi? Asema BWANA; hamtatetemeka mbele za uso wangu; mimi niliyeweka mchanga kuwa mpaka wa bahari, kwa amri ya daima, isiweze kuupita? Mawimbi yake yajapoumuka-umuka, hayawezi kushinda nguvu; yajapovuma sana, hayawezi kuupita.
[23]Lakini watu hawa wana moyo wa kuasi na ukaidi; wameasi, wamekwenda zao.
[24]Wala hawasemi mioyoni mwao, Basi, na tumche BWANA, Mungu wetu, aletaye mvua, mvua ya mwaka, na mvua ya vuli, kwa wakati wake; na kutuwekea juma za mavuno zilizoamriwa.
[25] MAOVU YENU YAMEYAGEUZA HAYA, NA DHAMBI ZENU ZIMEWAZUILIA MEMA MSIYAPATE.
[26]Maana katika watu wangu wameonekana watu waovu; huotea kama vile watu wategao mitego; hutega mtego, na kunasa watu.
[27]Kama tundu lijaavyo ndege, kadhalika nyumba zao zimejaa hila; kwa hiyo wamekuwa wakuu, wamepata mali.
Hiyo ni habari ya wana wa Israeli, ambapo Mungu alimtumia nabii Yeremia kutoa ujumbe juu yao, maana walifanya
machukizo mbele za Mungu.
Wakati Mungu alipokuwa anatembea na taifa hili, alilibariki sana, kwa sababu ni taifa alilokuwa amelichagua hivyo baraka ,neema zilikuwa juu yao kila jambo nzuri aliliweka juu yao
tusome
Kumbukumbu la Torati 33:28-29
[28]Na Israeli anakaa salama,
Chemchemi ya Yakobo peke yake,
Katika nchi ya ngano na divai;
Naam, mbingu zake zadondoza umande.[29]U heri, Israeli.
Ni nani aliye kama wewe, taifa lililookolewa na BWANA!
Ndiye ngao ya msaada wako,
Na upanga wa utukufu wako;
Na adui zako watajitiisha chini yako,
Nawe utapakanyaga mahali pao pa juu.
lakini tunajifunza tena kuna jambo ambalo lilikuja kubadilisha baraka hizo na kuwa laana, na sababu iliyosababisha ilikuwa sababu ya maovu yao kuzidi, na si kwamba maovu yale waliyafanya pasipo kujua walifahamu kabisa maana Bwana alipokuwa anatembelea nao aliwapa maagizo na sheria juu ya kuishi maisha ya utakatifu na ukamilifu hili kwamba kulinda baraka na neema hizo
Mambo ya Walawi 18:22-30
[22]Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo.
[23]Wala usilale na mnyama ye yote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; ni uchafuko.
[24]Msijitie unajisi katika mambo hayo hata mojawapo; kwa maana hizo taifa nitakazozitoa mbele zenu zimekuwa najisi kwa mambo hayo yote;
[25]na hiyo nchi imekuwa najisi; kwa ajili ya hayo naipatiliza uovu wake juu yake, na hiyo nchi yatapika wenyeji wake na kuwatoa.
[26]Kwa hiyo mtazishika amri zangu na hukumu zangu, wala msifanye machukizo hayo mojawapo; yeye aliye mzalia, wala mgeni aketiye kati yenu;
[27](kwa kuwa hao watu wa nchi wameyafanya machukizo haya yote, hao waliotangulia mbele zenu, na hiyo nchi imekuwa najisi;)
[28]ili kwamba hiyo nchi isiwatapike na ninyi pia, hapo mtakapoitia unajisi, kama ilivyoitapika hiyo taifa iliyotangulia mbele yenu.
[29]Kwani mtu awaye yote atakayefanya machukizo hayo mojawapo, nafsi hizo zitakazoyafanya zitakatiliwa mbali na watu wao.
[30]Kwa ajili ya hayo yashikeni mausia yangu, ili kwamba msifanye kabisa desturi hizi zichukizazo mojawapo, zilizotangulia kufanywa mbele zenu, wala msijitie unajisi katika mambo hayo; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.
Umeona hapo si kwamba Mungu akuwapa maagizo, bali aliwapa ili kwamba zile baraka zisiondoke juu yao, lakini kutokana na ugumu wa mioyo yao bado walimtenda tu Mungu uovu, ndipo hapo Mungu akampa ujumbe mtumishi wake nabii Yeremia kuwa
“Maovu yenu yameyageuza haya, na dhambi zenu zimewazuilia mema msiyapate.”
sababu ya maovu kuzidi ikapelekea hata zile baraka ziondoke juu yao
Sasa habari hii inatufundisha nini na sisi watu wa kipindi hiki, kama maandiko yanavyosema agano la kale ni kivuli cha agano jipya, hivyo basi habari hii inatufundisha nasi kuwa Mungu wetu alipo tuumba sisi wanadamu kitu cha kwanza aliachiliwa baraka kwetu nyingi tu, wala hakumumba mtu kwa kumkomoa bali alimfanya mtu kwa mfano wake hili kwamba kusudi lake litimie la sisi kumtumikia yeye na kumwabudu yeye kwa matendo yake makuu kwetu
Sasa swali la kujiuliza, imekuwaje sasa hivi mambo mengi yamekuwa tofauti na mipango ya Mungu kama alivyoweka hapo mwanzo alipotuumba tukizama zile baraka, neema,mvua kwa wakati wake nk…hazipo tena, badala yake imebadilika na kuwa tofauti kabisa, na mpango wa Mungu kwetu badala yake
magojwa yamekuwa mengi, vita ,njaa, uchumi kushuka, matetemeko, ukame,nk… mambo haya yamepelekea hadi watu kusema kuwa “Mungu ametuacha”, lakini kumbe si sahihi kabisa kusema neno hilo kwa sababu,
Mungu wetu siku zote anatembea na neno lake
hebu tusome andiko hili
Kumbukumbu la Torati 28:12-17
[12]Atakufunulia BWANA hazina yake nzuri, nayo ni mbingu, kwa kutoa mvua ya nchi yako kwa wakati wake, na kwa kubarikia kazi yote ya mkono wako; nawe utakopesha mataifa mengi, wala hutakopa wewe.
[13]BWANA atakufanya kuwa kichwa, wala si mkia; nawe utakuwa juu tu, wala huwi chini; utakapoyasikiza maagizo ya BWANA, Mungu wako, nikuagizayo hivi leo, kuyaangalia na kufanya;
[14]msipokengeuka katika maneno niwaamuruyo leo kwa lo lote, kwenda mkono wa kuume wala wa kushoto, kwa kuifuata miungu mingine na kuitumikia.
[15]Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya BWANA, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata.
[16]Utalaaniwa mjini, utalaaniwa na mashambani.
[17]Litalaaniwa kapu lako na chombo chako cha kukandia.
Umeona hapo ukianzia mstari wa kumi na mbili,hapo tunaona Bwana Mungu anatoa baraka kwa watu wake, lakini hapo katika mstari wa 15 Mungu mwenyewe kwa kinywa chake anasema kama usipotaka kusikiliza na kufuya maagizo yake zile zote baraka zitageuka na kuwa laana.
Tunajifunza nini nasi
Jambo ambalo Mungu anahitaji tulifahamu na tulijue sisi wanadamu wa kipindi hiki, ni kwamba Mungu siku zote analitazama neno lake hili kutimiza ahadi zake, na ikiwa watu wataenda sawa sawa maagizo yake basi baraka zitakuwa juu yao na endapo wataenda kinyume hapo ni laana tu, basi yapi twapaswa kuzingatia hili kutunza baraka zetu.
Lazima kila mmoja atambue nini kusudi la kuwepo hapa duniani, lazima utambue kuwa pasipo neno la Mungu huwezi kuishi maisha ya kumpendeza Mungu, hivyo ni lazima usome biblia maana huko ndipo yanapatikana maagizo yote, hapo ndipo tutafahamu umuhimu wa kumpokea Yesu Kristo maisha mwetu, na nini maana wakovu, na nini maana ya ubatizo, na ni kwa namna gani mtu ataishi maisha ya kumpendeza Mungu nk…yote hayo hayapatikani katika vitabu vya kawaida vya ulimwengu huu bali yanapatikana katika biblia takatifu na mtu anayafamu yote pale atakapo soma au kusikiliza
sasa vitu hivyo tukivifahamu ndiyo vinatusaidi kutunza baraka zetu
maana tutaishi maisha ya kumpendeza Mungu
Lakini ikiwa kinyume na hapo
ikawa watu watatenda uovu hakika baraka haitaonekana, hivyo ni lazima mambo kama haya yaondoke ndani yetu mfano
wizi, ufisadi,ulevi, unafiki,uongo,chuki,ndoa za jinsia moja, ushoga, kujibandili umbo, kuweka vitu bandia mwilini, ibaada ya sanamu, Udini nk… vitu hivi vikiondoka ndani yetu kisha tukaruhusu Neno la Mungu liwe ndani yetu hakika tutafurahia UKUU WA MUNGU NA UWEZA WAKE JUU YETU
Hivyo basi tufahamu leo na tutambue kwamba mambo maovu yanageuza baraka kuwa laana ndiyo maana leo tunashuhudia magojwa yakutisha, matetemeko, ukame, mvua za msimu kuchelewa, njaa nk… Ukiona mambo kama hayo yanatokea ebu rudi katika Neno la Mungu hili ujifunze nini wapaswa kufanya hili kurekebisha hali hizo, usikimbilie kusema Mungu ametuacha, jihakiki mwenyewe kwanza je nani wa kwanza kumwacha mwenzake. Na ukapokapo fahamu basi utajua nini wapaswa kufanya hili kurejesha baraka, na tutakapo kunyenyekea na kutubu maovu yetu hakika Bwana Mungu atatusamehe maana
neno la Mungu linasema
Isaya 1:18-20
[18]Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.
[19]Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;
[20]bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa cha BWANA kimenena haya.
Baba yangu, mama, kaka, dada neno la Mungu ndiyo taa ya miguu yetu endapo tusipolifuata tutaangukia pabaya , maovu yamezidi wanadamu hebu tugeuke leo na tuifikie toba unaishi maisha ya dhambi, wokovu wa uvuguvugu acha leo na ulitazame neno la Mungu nini unapaswa kufanya, duniani Mungu hakukuumba uje utende uovu bali alituumba tumtukuze kwa matendo yake kwetu.
Tambua kuwa
maovu yetu ndiyo yanabadilisha baraka zetu kuwa laana
ikiwa bado ujaokoka basi ni vyema kuchukua hatua hiyo jema hili ujue kusudi la wewe kuwepo hapa duniani, maana uwezi kulijua sehemu nyingine ila ni Kwa Bwana wetu Yesu Kristo mwamini leo
Bwana wetu anarudi tujihakiki maisha yetu
Barikiwa.